Baada ya kufanyika nchi tofauti duniani, FOSS4G2018 inakuja Tanzania. Hii ni kusema kwamba Africa kwa ujumla tunaungana pamoja kuonyesha na kujadiri kazi za utengenezaji na utumiaji wa reamani katika miji yetu kwa ajiri ya maendeleo endelevu. FOSS4G yenye kirefu chake “Free and Open Source Software for Geographic” ni mfululizo wa makongamano ambayo huandaliwa na OSGEO tangu mwaka 2002 ambayo hufanyika kila mwaka na kukutanisha wana geographia kutoka duniani kote watumiaji wa program zisizo za kulipia (OSGEO) kwa ajiri ya kutambua fursa na changamoto zilizopo katika mipango na uendelezaji wa mji unaoshirikisha Jamii.
Mfururizo huu wa makongamano ulianza rasmi kufanyika tangu mwaka 2002 na kushika kasi mwaka 2006 kama mwanzo wa makongamano kwenye nchi mbalimbali katika mabara ya Ulaya, Amerika, na Asia.
Mwaka 2018 kongamano hili ambalo litaleta zaidi ya watu 800 kutoka nchi mbalimbali duniani litafanyika Dar es salaam, Tanzania. Nikiwa kama Mwenyekiti wa kongamano nikishirikiana na mwenyekiti mwenzangu Mark Iliffe, baada ya kuandaa timu ambayo tulikaa na kuandika kuomba kongamano lifanyike Dar es salaam. Nia na mathumuni ni kukuza utumiaji wa ramani na kuunganisha watumiaji wa ramani ili pamoja kutatua matatizo yanayoikumba jamii. Baada ya mchakato wa uchaguzi, OSGeo ilichagua kongamano hilo lifanyike Dar es salaam kwa iyo tumewashinda wapinzani wetu ambao ni Thailand na Peru.
Kufanyika kwa kongamano la FOSS4G 2018 Dar es salaam litasababisha sio tu utalii wa Tanzania bali kujadili, kuonyesha na kusaidia maendeleo ya Tanzania na Africa kwa ujumla.
Mimi nina furaha kwa kongamano hili kufanyika Dar es salaam, kwa iyo tukutane mwakani (2018) kwa kongamano.